Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mheshimiwa Halima Dendego ameagiza kukabidhiwa majina ya waliokopa Benki ya Wananchi wa Tandahimba (TACOBA) wakashindwa kurudisha. Miongoni mwa wakopaji hao wamo wanasiasa na viongozi wa kijamii. Agizo hilo amelitoa katika kikao cha mwaka cha wanachama wa Benki hiyo kilichofanyika uwanja wa michezo wa Tandahimba jana.
Mkuu
wa Mkoa wa Mtwara Mheshimiwa Halima Dendego akizungumza na wanachama cha Benki
ya Wananchi wa Tandahimba (TACOBA)
Katika kikao hicho ambacho pia, kilikusudia
kuchagua uongozi mpya wa TACOBA, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki
hiyo aliyemaliza Muda wake, Manase Ndoroma alibainisha changamoto na ushauri
kwa mambo matano ambayo aliwataka wadau kuyafanyia kazi likiwemo la wanasiasa
na viongozi mbalimbali kushindwa kurudisha mikopo yao na hivyo kuathiri
utendaji wa Benki.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi
wa Benki ya Wananchi wa Tandahimba anayemaliza Muda wake Manase Ndoroma akiwasilisha taarifa
ya utekelezaji wa majukumu yao kwa kipindi cha uongozi wao.
Mwenyekiti huyo ambaye
ameiongoza Bodi kwa miaka 6 ameshauri Ukaguzi
ufanyike mara kwa mara ili Benki Kuu iweze kubaini kwa haraka mapungufu
kabla athari zake hazijawa kubwa. Aidha Pale palipo na Benki za aina hii
Mamlaka za Serikali za Mitaa zielekezwe kufungua akaunti kwenye Benki hizi, pia
Serikali iziagize Halmashauri zote zenye Benki
za aina hii kwenye maeneo yao, asilimia tano ya wanawake na tano ya
vijana zinazotengwa na Halmashauri kila mwaka ziingizwe kwenye Benki hizi.
Ushauri wa mwisho aliitaka
serikali ifanye uamuzi wa kuzitaka Halmashauri zote zilizo na benki hizo
akaunti zao zote zifunguliwe katika Benki hizi.
Akisisitiza suala la kukopa
bila kulipa Mheshimiwa Dendego ambaye amekuwepo katika nafasi hiyo kwa miaka
miwili sasa amesema hakuna njia nyingine ya kuendeleza Benki ikiwa wakopaji
hawarudishi mikopo yao. Amesema wakopaji wote ndani ya mkoa wa Mtwara wako chini
yake yeye kama Mkuu wa Mkoa, hivyo anawajibu wa kuhakikisha wanarudisha.
‘Kwa
Wale wenzetu watawala. Kama ushahidi upo, orodha tunayo kuwa walikopa katika Benki
hii na bado wanapumua wakiwa hawajarudisha pesa zetu, naomba wawekwe wazi. Mimi
mwenyewe nitasimama kidete kuhakikisha wanarudisha. Kama ni wanasiasa mimi ndiye
mwanasiasa kabisa katika mkoa huu, na wananchi wa kawaida mimi ndiyo Mkuu wao wa
Mkoa. Hatutakubali kurudishwa nyuma’. Amesema.
Mwenyekiti
anayemaliza Muda wake Manase Ndoroma akimkabidhi MKuu wa Mkoa wa Mtwara
Mheshimiwa Halima Dendego cheti cha utambulisho wa Mwanahisa.
Katibu
wa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Said Nguyu akipokea Cheti cha uanachama kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa
Mtwara Halima Dendego baada ya kununua hisa katika Benki hiyo.
Katika mkutano huo
Mheshimiwa Dendego ameendesha Harambee ya kununua hisa ambapo zilipatikana hisa
21,509 Huku yeye mwenyewe akiwa wa kwanza kuongeza hisa 500 kutoka hisa 500
alizokuwa akimiliki kabla.
Mmoja wa wanahisa wa Benki
hiyo Lucy Ogutu ambaye pia ni mwakilishi wa ITV Mtwara, akipokea cheti cha
Mwanahisa.
Kaimu
katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji Sekretarieti ya Mkoa wa Mtwara,
Amani Rusake akitoa ahadi ya kununua hisa 200.
Aidha, Mheshimiwa Dendego
amevitaka Vyama vya Msingi Mkoani Mtwara kuhifadhi Benki angalau asilimia 20 ya
fedha zinazotokana na mapato yao ya musimu husika ili kujiandaa na musimu
unaofuata.
Wanahisa
wa Benki ya Wananchi wa Tandahimba wakifuatilia hoja zinazotolewa na viongozi
wao.
TACOBA ni Benki pekee ya
wananchi katika mkoa wa Mtwara ambayo ilianzishwa mwaka 2009. Hisa moja ya
Benki hii inauzwa shilingi 1000.
No comments:
Post a Comment