MTWARA RS

FUATILIA TAARIFA MBALIMBALI ZINAZOHUSU MKOA WA MTWARA NA SEHEMU NYINGINE NDANI NA NJE YA TANZANIA, KWA MAWASILIANO E-mail: yustace.evaristy@mtwara.go.tz SIMU: +255 717 697 205

Thursday, 19 March 2020

Miradi hii ni fahari ya Mtwara


Mandhari ya kupendeza imeanza kuonekana ndani ya Manispaa ya Mtwara Mikindani kufuatia utekelezaji wa mradi wa Ujenzi na Uendelezaji wa Miji ya Kimkakati Tanzania (TSCP). Mradi huu unatarajiwa kukamilika Mwezi Mei mwaka huu na utagharimu shilingi bilioni 21.6. 

Fedha hii ilitolewa kwa mkopo kutoka Benki ya Dunia kipindi cha awamu ya Nne ya uongozi. Mwaka 2018 Benki hiyo iliamua kuongeza mkopo huo baada ya kuridhishwa na mipango ya utekelezaji kupitia serikali ya awamu ya tano. 

Moja ya eneo linalotekelezwa katika mradi huo ni ujenzi wa bustani za mapumziko (Recreation Centres). Bustani hizi zimejengwa katika maeneo ya Maduka makubwa, eneo ilipokuwa Tilla Bar pamoja na Uwanja wa Mashujaa.  
Hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa Bustani ya mapumziko  eneo la maduka makubwa.
Bustani ya maduka makubwa itakavyokuwa baada ya kukamilika

Hatua iliyofikiwa katika ujenzi Bustani ya mapumziko Tilla

UWANJA WA MASHUJAA.     

Kabla ya mpango wa ujenzi, uwanja wa mashujaa ulikuwa ukitumika kwa shughuli za mikutano na matamasha mbalimbali. Mpango mpya wa ujenzi umelenga kulifanya eneo hilo liwe eneo la mapumziko na michezo mbalimblali. Baadhi ya mambo mazuri yaliyoko katika mradi huo ni mabwawa ya kuogelea (swimming pool), viwanja vya michezo ya Watoto, viwanja vya mpira wa wavu (Basketball) na mpira wa kikapu (volleybal).  Pia maeneo ya huduma za vinywaji na mengine mengi. Pia kutakuwa na mnara wa kumbukumbu ya mashujaa ili kuwaenzi mashujaa waliopigana kuikomboa Tanzania na nchi jirani.

Mnara wa Kumbukumbu ya mashujaa unaendelea kufanyiwa maboresho.

Ujenzi wa Bwawa la kisasa unaendelea katika Bustani ya Mashujaa
Ujenzi wa uwanja wa mpira wa kikapu unaendelea.

Mradi utaongeza mapato kwa halmashauri na kuwapa fursa ya mapumziko yenye tafakari nzuri ya siku baada ya muda wa kazi.

SOKO LA CHUNO
Eneo lingine lililoko katika mradi huu ni ujenzi wa soko la kisasa maarufu kama Soko la Chuno.
Hatua iliyofikiwa katika uenzi wa soko la Chuno
Soko hili linatarajiwa kuwa na vizimba 193 vya biashara, bucha nane, vyumba vinne vya ofisi, sehemu Nne za kuuzia vyakula, vyoo vinne, stoo saba, sehemu kwa ajili ya mashine za kutolea fedha (ATM) na sehemu ya matangazo. Vilevile kutakuwa na sehemu saba za kushushia mizigo na sehemu mbili za maduka ya jumla. Pia eneo la maegesha ambalo litakuwa na uwezo wa kuegesha magari 81 kwa wakati mmoja.
Muonekano wa soko baada ya kukamilika
Matumaini makubwa ni kwamba soko hili litawezesha halmashauri kuwa na chanzo endelevu cha mapato ya ndani huku wananchi wakifaidika kwa kupata ajira na kuwekeza katika sko hilo. Ujenzi wa soko hili unatarajia kugharimu shilingi bilioni 4.8.
MIFEREJI YA MAJI
Eneo lingine ni ujenzi wa mfereji wa maji ambao utagharimu shilingi bilioni 3.5. Mfereji huu  wenye urefu wa km. 3.4 umejengwa kuanzia maeneo ya wafanyabishara mtaa wa Skoya kupitia Nabwada, Shakuru, Mtepwezi hadi Baharini. Pia mifereji midogomidogo ya kukusanyia maji ya mvua katika maeneo ya maduka makubwa, reli na vigaeni ambayo yote kwa pamoja imewezesha wananchi wa Manispaa Mtwara Mikindani kuepukana na adha ya kuhama makazi yao kipindi cha mvua.
Mradi huu pia umegusa ujenzi wa kituo cha daladala cha Mikindani, barabara za lami maeneo mbalimbali ndani ya manispaa pamoja na dampo la kisasa.

Licha ya kuufanya mji wa Mtwara kuwa moja ya miji ya kuvutia, miradi hii itaongeza mapato kwa halmashauri na wananchi kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment