Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe. Sebastian Waryuba amepiga marufuku
michango inayokwenda kinyume na maagizo yaliyoko katika miongozo ya elimu shuleni.
Agizo hilo amelitoa jana Februali 24, 2020 kufuatia malalamiko ya wananchi wakati wa ziara yake ya siku moja kusikiliza kero za wananchi na kukagua maendeleo ya shule. Wananchi hao walidai kuwa baadhi ya shule hasa za sekondari walimu wamekuwa wakiomba michango ambayo inaleta usumbufu kwa wazazi.
Mhe. Sebastian Walyuba akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mmeda
Mheshimiwa Walyuba amesema michango inayokwenda kinyume na utaratibu inaweza
kuwa chanzo cha wanafunzi kushindwa kuhudhuria shuleni na kwamba inapingana na dhana
ya elimu bila malipo inayotekelezwa na serikali ya awamu ya Tano kupitia kwa
Rais, Dkt. John Pombe Magufuli.
Katika ziara hiyo ya siku moja Mhe. Walyuba alitembelea vijiji vya Mmeda,
Mabeti na Mkola akiwa amembatana na maafisa wa halmashauri, wataalam wa TANESCO
na TARULA. Aidha, alihimiza Amani, kufanya kazi kwa bidi na kuwataka wazazi
ambao Watoto hao hawajaripoti shuleni wakamatwe na kufikishwa mahakamani.
Mhe. Waryuba akihamasisha wanafunzi kuwa raia wema kupitia mafunzo ya darasani shule ya Msingi Mmeda
wananchi wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Sebastian Walyuba. (hayupo pichani)
No comments:
Post a Comment