MTWARA RS

FUATILIA TAARIFA MBALIMBALI ZINAZOHUSU MKOA WA MTWARA NA SEHEMU NYINGINE NDANI NA NJE YA TANZANIA, KWA MAWASILIANO E-mail: yustace.evaristy@mtwara.go.tz SIMU: +255 717 697 205

Thursday, 27 September 2018

Waziri Kalemani awataka watanzamia kutumia Kifaa cha Umeme Tayari. Hakihitaji 'Wiring'


Waziri wa Nishati Mheshimiwa Dkt. Medard Kalemani amewaka watanzania  kuchangumkia fursa iliyotolewa na serikali ya kuuunganishiwa umeme kwa kutumia kifaa kinachojulikana kama Umeme Tayari (UMETA). Amesema kifaa hicho kinamuepusha mtumiaji na gharama za kufanya ‘wiring’ na hivyo kupunguza gharama za kuingiza umeme kwenye nyumba.
Waziri ameyasema hayo jana katika maeneo tofauti alipokuwa katika ziara yake ya siku mbili mkoani Mtwara.

“Serikali imeamua kuwapungumzia gharama wananchi kwani ukishaweka hicho chombo hulazimiki tena kufanya ‘wiring’ kwa nyumba za wastani, hasa nyumba zenye chumba kimoja hadi vinne.  Kwa vile hicho kifaa kinafaa kwa matumizi yote isipokuwa viwanda tunawashauri wnanchi wavitumie. Pia tunashauri vifaa hivi vitumike kwenye taasisi za Umma kama ofisi za vijiji vituo vya afya, vituo vya polisi, zahanati na maeneo mengine ambayo kimsingi si lazima sana ufanye wiring.”
Amesisitiza kwamba serikali imewataka wakandarasi wahakikishe wanavitoa kwa wateja wa kwanza mia moja hadi mia mbili hamsini. baada ya hapo vinakuwa vinauzwa kwa bei ya serikali ambayo ni shilingi 36,000.

Kwa kuanzia amegawa vifaa hivyo katika majimbo yote aliyotembelea ikiwemo Nanyamba, Newala na Lulindi.

Pamoja na punguza hilo amesema serikali bado inaendelea na punguza la kuingiza umeme kupitia mradi wa REA ambapo gharama yake ni shilingi elfu 27 tu kwa maeneo ya vijijini.

No comments:

Post a Comment