Mhe. Byakanwa akionesha moja ya nyumba ya Mwalim katika shule ya Msingi LulindiMoja ambayo nyavyu za madirisha zimeharibika bila kufanyiwa matengenezo
Mheshimiwa Byakanwa amesema hatavumilia mwalimu anayepewa nyumba bure kushindwa kuitunza. Anasema ni bora nyumba hiyo akapewa mwalimu mwingine mwenye moyo wa kuitunza kuliko Mwalimu anayesubiri serikali imfanyie kila kitu.
Amesisitiza kuwa
serikali imeonesha kujali ndiyo maana imewajengea nyumba na kuwapa waishi bure
hivyo haipendezi mwalimu anayeishi katika nyumba hiyo kuendelea kusubiri
serikali irekebishe mambo madogomadogo ikiwemo nyavu za madirisha zilizochoka.
Licha ya agizo
hilo Mheshimiwa Byakanwa ameahidi kuchangia bati za vyumba vitatu vya madarasa kwa
sharti la kuwataka wanakijiji kuhakikisha wanajenga boma. Pia ameitaka serikali
ya kijiji hicho kuandaa tofari za kutosha nyumba mbili za walimu ambapo
amemutaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Juma Satma kuchangia ujenzi
wa nyumba hizo.
Kwa upande wake
Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Juma Satma
amesema agizo hilo wamelipokea na kwamba wako tayari kulifanyia
utekelezaji.
Awali akiwasilisha
kero ya shule hiyo Rajab Abdelimali Soni, mkazi wa kijiji hicho alimuomba Mkuu
wa Mkoa kutembelea shule hiyo kutokana na changamoto ya miundombinu ya shule
hiyo.
Amesema shule
hiyo ni kongwe lakini bado inatatizo la miundombinu ya nyumba za walimu pamoja
na vyumba vya madarasa jambo ambalo limekuwa likisababisjha walimu kuishi mbali
na mazingira ya shule na hivyo kuathili utendaji kazi.
No comments:
Post a Comment