Anaandika Karl Weule kwenye kitabu chake ‘Native Life in East Africa.’ Tafsiri ya Kiingereza kutoka kijerumani imetolewa na Alice Werner. Kimechapishwa mwaka 1909 na New York D’ Appleton and Company. Tafsiri ya Kiswahili isiyo rasmi inatolewa na Evaristy Masuha.
Karl Weule
Anaanza Weule kwa
kusimulia.
Niliingia Newala Mwishoni
mwa Septemba 1906. Kubwa lililonishangaza ni hali ya maisha ya wakazi wa Mji
huu ambao wanaishi katika mazingira ya shida kubwa ya maji. Mimi na mwenzangu Knudsen
tulijiuliza maswali kwa nini watu hawa wamekuwa na ujasili wa kuishi katika
misitu mikubwa yenye shida ya maji kiasi hiki.
Hata hivyo nilipata picha
halisi ya simulizi niliyokuwa nayo tangu nikiwa ujerumani juu ya mapori makubwa
yenye wanyama hatari ambayo yamewazunguka watu wa Ujerumani ya Afrika Mashariki.
(German East Africa).
Wakati tunaingia mji huu tumetembea
umbali mrefu tukipita mapori makubwa. Ishara ya uwepo wa watu katika eneo
tulilokuwa tukilikaribia ni sauti za shoka na mapanga yakiangusha misitu
mikubwa. Kazi hii ilikuwa inafanywa na wanafamilia wote ikiwemo baba, mama,
watoto, na wakwe.
Huu ndio utaratibu wa
kilimo cha watu hawa, kufyeka kisha kuchoma moto. Baada ya kuteketeza msitu,
wenyeji hawa hupanda mazao tayari kwa kupalilia hadi kuvuna.
Wamakonde
na tamaduni ya kuzika wafu wao wima.
Baada ya kuwapata wenyeji
katika eneo hili ambalo tulitambulishwa kuwa linaitwa Mahuta, utafiti wangu
ulianzia kutaka kujua kwa nini wanakuwa na ujasiri wa kuishi katika maeneo haya
yenye hatari ya wanyama na shida kubwa ya maji.
Mwenyeji wangu alinieleza
kuwa ipo historia ndefu ambayo inawafanya wasiishi katika maeneo ya maji.
Alieleza kuwa simulizi walizozipata toka kwa babu zao ni kwamba kabla ya kuwa
kijiji eneo hilo lilikuwa pori lenye msitu mkubwa na wanyama wakali. Mwanzo wa
maisha katika mji huo ulianza baada ya ujio wa mtu mmoja aliyetokea kusikojulikana.
Mtu huyo alikuwa na nywele nyingi ambazo zilikuwa hazichanwi. Pia alikuwa
akioga mara chache na kula kidogo sana.
Baada ya kuanzisha makazi
yake pale Mahuta mtu huyo alichonga kinyago cha mwanamke ambacho alikisimamisha
katikati ya mji wake. ilipokuwa inafika usiku, kinyago au sanamu hiyo ilikuwa ikibadilika
kuwa mwanamke ambaye walikuwa wakitelemka naye mto Ruvuma kwa ajili ya kuoga na
kuchota maji.
Baada ya muda mwanamke huyo
alizaa mtoto wa kiume kisha wawili hao wakaamua kuhamisha makazi yao. Wageni
hao walitembea hadi wakavuka mto Mbemkuru ambapo yule mama alizaa mtoto wa pili
akiwa amefariki.
Hali hiyo iliwasikitisha wageni
hao wakalazimika kurudi Mahuta ambapo walizaa tena mtoto wa tatu. Mtoto huyu
alikuwa na kuishi akiwa na afya njema. Baada ya muda familia hiyo ilipanuka na
kutengeneza ukoo ambao waliuita ‘Wamatanda’. Wamatanda hawa walipokuja
kuongezeka ukatokea ukoo ambao nao ulipanuka na kujiita wamakonde.
Mwenyeji wangu aliendelea
kuwa huyo Babu asiyenyoa nywele alipofikia siku za mwisho wa maisha yake,
alitoa agizo kwa watoto wake kuhakikisha wanawazika ndugu zao kwa kuwasimamisha
wima kaburini ikiwa ni kukumbuka ya asili ya bibi yao (sanamu iliyokuwa ikipata uhai usiku). Pia akawapa onyo wasikae
karibu na mto au kwenye chanzo chochote cha maji.
Aliwaeleza kuwa mauti ya binadamu yamejaa na
yanaishi kwenye chanzo cha maji hivyo wasithubutu kuishi maeneo kama hayo. Hali
hiyo ndiyo iliwafanya waendelee kuishi hapo Mahuta.
Tafadhali Toa comment yako hapo chini
Kweli tumetoka mbali katika tamaduni zetu
ReplyDeleteThis comment has been removed by the author.
DeleteOK, NIMEPATA FAIDA KUJUA HISTORIA
ReplyDeleteASANTE
Je historia ya vinyago vya komakomde imetokea wapi, nashukuru sana
ReplyDelete