MTWARA RS

FUATILIA TAARIFA MBALIMBALI ZINAZOHUSU MKOA WA MTWARA NA SEHEMU NYINGINE NDANI NA NJE YA TANZANIA, KWA MAWASILIANO E-mail: yustace.evaristy@mtwara.go.tz SIMU: +255 717 697 205

Sunday 13 August 2017

RC Mtwara alivyotunukiwa tuko ya Mwanamke Jasiri.



Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania Dayosisi ya Kusini Mashariki Usharika wa Kanisa Kuu wamemtunuku Tuzo ya Mwanamke Jasiri Mkuu wa MKOA wa Mtwara. Mhe. Halima Dendego ikiwa ni kutambua mchango wake Mkubwa ktk kusukuma maendeleo ya Mtwara.

Tuzo hiyo iliyotolewa Jana katika kanisa la KKKT lililoko Mjini Mtwara lilishuhudiwa na viongozi mbalimbali wa mkoa pamoja na waimbaji kutoka makanisha mbalimbali ikiwemo kwaya ya Kanisa Katoliki Parokia ya Mtwara.

Akizungumza wakati wa kumkabidhi tuzo hiyo, Askofu Mkuu wa Dayosisi hiyo, Lucas Mbedule Juda  amesema vipo vielelezo vya mambo mengi makubwa aliyoyafanya Mhe. Dendego ambayo ni kielelezo cha ujasiri wake katika kusimamia haki.


Amesema yeye mwenyewe Askofu amekuwa mfuatiliaji wa karibu wa kazi za Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa tangu akiwa Mkuu wa Wilaya ya Tanga kabla ya kuhamishiwa hapa Mtwara miaka mitatu iliyopita.


Akinukuu maandiko matatatifu kutoka kwenye kitabu cha “Marko 16.1-4 Mbedule amesema kitabu hicho kinaonesha ujasiri mkubwa unaohitajika katika kuitafuta haki jambo ambalo Mheshimiwa Dendego ameliweza.


“Hata sabato ilipokwisha kupita, mariamu Magdalena na Mariamu mamaye Yakobo, na Salome walinunua manukato wapate kwenda kumpaka. Hata alfajili mapema siku ya kwanza ya juma, wakaenda kaburini, jua lilipoanza kuchomoza. Wakasemezana wao kwa wao, ni nani atakayetuviringishia lile jiwe mlangoni pa kaburi? Hata walipotazama, waliona ya kuwa lile jiwe limekwisha kuviringishwa, nalo lilikuwa kubwa mno.”


Anasema andiko hilo linawataja baadhi ya watu ambao ni maarufu kwa kukatisha tamaa wenzao katika jitihada za mapambano ya ukombozi kama ambavyo mmoja wa wanawake hao alivyojaribu kuwakatisha tamaa wanawake wenzake lakini ujasili wa wale akina mama haukukatishwa tamaa katika kuliendea jiwe lililofunika mwili wa Yesu.


Akizungumzia hati aliyoitoa Askofu Mbedule amesema hati hiyo inatambulika kama HATI YA ASKOFU YA HESHIMA YA JUU ambayo hutolewa Mara chache, kwa watu wachache hasa baada kujiridhisha na utendaji uliotukuka kwa mhusika.

Kwa upande wake Mhe. Dendego ambaye amekuwa Mkuu wa MKOA huu kwa miaka mitatu sasa anasema tuzo hiyo imempa nguvu ya kuendeleza jitihada zake kutetea maslahi ya wengi hasa wanyonge. Amesema wapo watu wengi ambao wamekuwa wakimkatisha tamaa katika jitihada zake. Wengine wamekuwa wakimbeza na hata kumsingizia vitu vingi lakini kwa heshima aliyopewa na kanisa hilo imempa nguvu na anajiona ni mpya katika mapambano.


Mheshimiwa Dendego amewataka akina mama wengine wajipe moyo wa mapambano kwani katika kufikia ushindi lazima mtu ajitowe mhanga.

Kwa upande wao wananchi waliokuja kushuhudia tukio hilo wamepongeza uamuzi wa kanisa hilo kwamba umefanyika katika muda muafaka na kwa usahihi kabisa. 


Mwalimu Frank Komba wa shule ya Msingi magomeni Mkoani Mtwara anasema amekuwa akifuatilia kwa karibu kazi za Mkuu wa Mkoa tangu amekuwepo hapa na amefurahishwa na mambo mengi likiwemo suala la kusimamia elimu huku akiwabana wananfunzi wanaopata ujauzito na wanaowapa. Anamshauri Mkuu huyo aendelee na jitihada hizo kwani nidhamu kwa wanafunzi imejengeka sasa. 



Joseph Haule Mkazi wa Mangamba Mtwara mjini anaongeza kuwa Mkuu wa Mkoa ameweza kuzuia suala la kuwatumikisha watoto wa kike katika mtindo wa wafanyakazi wa ndani na hata wakati mwingine kuwageuza chombo cha starehe. Amemtaka Mheshimiwa Magufuli aendelee kumuunga mkono na asimuhamishe mkoani Mtwara.

Aidha Viktoria Daudi mkazi wa Mtwara anaguswa na kazi za Mkuu wa Mkoa katika suala la usimamizi mzuri wa zao la Korosho. Anasema kabla yake kulikuwa na ukiukwaji wa taratibu za ununuzi na uuzaji wa korosho ambapo wanunuzi wengi walikuwa wakinunua korosho katika mfumo usio rasmi na hivyo kuwanyima mapato stahili wakulima. Baada ya usimamazi wa Mheshimiwa Dendego suala hilo limepungua kwa kiasi kikubwa na sasa wananchi wanafurahia mfumo wa stakabadhi ghalani.

Video hiyo hapo chini.



No comments:

Post a Comment