MTWARA RS

FUATILIA TAARIFA MBALIMBALI ZINAZOHUSU MKOA WA MTWARA NA SEHEMU NYINGINE NDANI NA NJE YA TANZANIA, KWA MAWASILIANO E-mail: yustace.evaristy@mtwara.go.tz SIMU: +255 717 697 205

Monday 14 August 2017

RC Mtwara aagiza kusimamishwa MKuu wa Idara ya Ardhi Mtwara DC

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Mhe. Halima Dendego amemuagiza
Mkurugenzi wa Halmshauri ya Wilaya ya Mtwara Omari Kipanga kumsimaisha kazi
Mkuu wa Idara ya Ardhi Katika halmshauri hiyo, Denis Kitali kutokana na kukiuka
makubaliano ya idara ya ardhi na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa juu ya namna bora ya uendelezaji
wa eneo la viwanjwa Msijute kilipo kiwanda cha Saruji cha Dangote.


Akitangaza uamuzi huo katika kikao cha Baraza Maalum la Madiwani
la kujibu hoja za Mkaguzi Mkuu wa Fedha za Serikali (CAG), mkuu huyo amesema
licha ya kusimamishwa kazi, hatua nyingine za kisheria zitafuata dhidi yake.

Mheshimiwa Dendego amesema mpango wa kupima eneo hilo kwa
ajili ya viwanda ulifikiwa kwa makubaliano kati ya Ofisi yake na Halmshauri
hiyo ambapo mkuu huyo alishiriki kikamilifu tangu mwanzo.

Amesema kilichomshangaza ni Mkuu huyo kuwaeleza madiwani kuwa
vipo viwanja 380 ambavyo Halmashauri inampango wa kuviuza ili kuongeza mapato
ya halmashauri. Amesema hilo ni suala lisilokubalika na amekuwa akiwasiliana
naye kwa maneno na kwa maandishi zaidi ya mara tano akimuelekeza juu ya mpango
mzuri wa uendelezaji wa eneo hilo.

Aidha, Mhe. Dendego ameendelea kusisitiza kuwa kama yupo
kiongozi yeyote aliyekwisha chukua fedha azirudishe kwani msimamo wake ni huo
huo na hautabadilika. Amesema lengo lake ni kuwa na mji wa kisasa wa Mtwara.
wenye viwanda vinavyokwenda na mahitaji ya kisasa.

Nao baadhi ya madiwani wa halmashauri hiyo, akiwamo
Maupa Abdul na Ramadhan Mfaume wameelekeza lawama zao kwa idara ya ardhi ya
halmashauri hiyo kwa kutotimiza wajibu wao kikamilifu

Video yake Hiyo.


No comments:

Post a Comment