Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mheshimiwa Gelasius Gasper
Byakanwa ameahidi kutoa huduma bila kubagua kundi lolote katika jamii. Mheshimiwa
Byakanwa aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa huu Oktoba mwaka huu amesema Serikali
ya awamu ya Tano anayoitumikia imejikita kuhudumia watu bila kuangalia
itikadi zao, hivyo yeye kwa nafasi yake atahakikisha anawahudumia watu wote
bila kuangalia itikadi zao kwani misingi ya Umoja wa Watanzania hauendani na
itikadi za utengano wa imani yoyote bali Tanzania ni ya wote na umoja ndio
msingi wa watanzania.
Mheshimiwa Byakanwa ameyasema hayo wiki hii
wakati akizungumza na wazee maarufu pamoja na viongozi wa Dini kwenye kikao
kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Boma Mkoa.
Amesema anatambua changamoto mbalimbali
zinazowakabili wananchi wa Mkoa wa Mtwara ikiwemo suala la elimu hivyo amemuagiza
Katibu Tawala Mkoa aitishe kikao cha wadau wa Elimu ili kujadili kwa pamoja
changamoto hizo.
Kwa upande wa uhaba wa magunia ya kuuzia korosho
amewaagiza Bodi ya Korosho kuhakikisha wanasambaza kwa kila mkulima ili
isitokee yeyote akakossa gunia. Aidha msimamo wa kusafirisha korosho ghafi
kwenda nje ya nchi kupitia bandari ya Mtwara uko palepale.
Kwa Dondoo na mengi yaliyojiri katika kikao hicho
soma hapa.
*YALIYOJIRI
KWENYE KIKAO CHA MKUU WA MKOA WA MTWARA MHE: GELASIUS G. BYAKANWA NA WAZEE
MAARUFU PAMOJA NA VIONGOZI WA DINI JANA NOVEMBA 21, 2017 UKUMBI WA BOMA MKOA.*
-Amewashukuru wazee na viongozi kwa mahudhurio
makubwa kwani imempa faraja kuwa wenyeji wapo na wamempokea vema
-Ameahidi kukutana na viongozi hao kila
baada ya miezi sita kujadililiana masuala mbalimbali na kupeana mrejesho wa
yale yote yaliyojadiliwa kwenye kikao kilichopita
-Amewataka wataalamu kufanyia kazi ushauri
uliotolewa na wazee pamoja na viongozi wa DINI na kutoa majibu ya kisayansi
-Ametoa agizo kwa benki zote kutenga
dirisha maalumu la kuhudumia wazee, akina mama wajawazito na watu wenye
mahitaji maalumu
-Serikali ya awamu ya tano imejikita
kuhudumia watu bila kuangalia itikadi zao, "Naahidi nitahudumia watu wote
bila kuangalia itikadi zao nikiamini misingi ya Umoja wetu hayaendani na
itikadi hizo kwani Tanzania ni yetu, Umoja ni wetu"
-Wananchi muna jukumu la kutoa taarifa kwa
watu mnaowashuku kwenye maeneo yenu
-Naagiza Wakuu wa Wilaya, Watendaji wa
Mitaa/vitongoji kuwa na orodha ya wakazi kwenye maeneo yenu
-Amewataka wakurugenzi kuwasimamia wenyeviti wa
mitaa/kitongoji kila mmoja kwa nafasi yake ahakikishe ameorodhesha
Wananchi wanaoishi kwenye eneo lake wanaoanzia umri wa miaka 18 na kuendelea na
NDANI ya miezi 3 zoezi liwe limekamilika
-Amemuagiza Katibu Tawala Mkoa aitishe kikao cha
wadau wa Elimu ili kujadili kwa pamoja changamoto za elimu
-"Changamoto za watoto wa kike kupata
mimba shuleni nazitambua, kwenye kikao cha wadau tutaona njia bora ya kuboresha
Elimu"
-Ameagiza bodi ya korosho wahakikishe
magunia yanasambazwa kwenye maeneo yote
-Atahakikisha kila mkulima anapata gunia
litakalobeba korosho na si kitu kingine
-Serikali ya Mkoa tumeamua na tumesisitiza
wafanyabiashara wa korosho kutumia Bandari ya Mtwara
-Nimepata taarifa kutoka kwa Meneja wa Bandari
Mtwara kuwa hadi wiki iliyopita Bandari imekusanya Shilingi Bilioni 24
-Zao la korosho limetoa ajira nyingi kwa
wananchi wa Mtwara
-Ni utaratibu wa Serikali na maelekezo kuwa
Malipo yote ya wakulima wa korosho yatapitia Benki
-Amewaomba viongozi wa DINI na wazee waendelee
kutoa Elimu kwa Wananchi wetu wafungue akaunti Benki.
-Amewasisitiza wananchi kutoa Pesa kidogo kidogo
na wawe na utamaduni wa kuweka akiba
-Amewataka wakulima wanapoenda kutoa fedha Benki
watoe kulingana na mahitaji yao,ukibeba fedha nyingi unahatarisha maisha yako
-Tunapofurahia bei nzuri ya korosho nendeni
mkakate Bima ya Afya
-Wakurugenzi muna jukumu la kuniandalia
baada ya msimu kuisha wananchi wangapi wamejiunga kwenye Mfumo wa Bima ya Afya
-Amewataka wakulima kusomesha watoto wako kutoka
na na fedha za korosho
-Mkurugenzi wa Manispaa sitaki kuona watu
waancheza pool muda wa kazi wala pombe kuuzwa muda wa kazi
-Nitakaa na bodi ya Timu Ndanda na wadau
wanaotaka kuiendeleza Timu kwa pamoja tujadili Namba ya kuiendesha timu
hiyo ili iendelee kubaki kwenye ligi juu na vijana wetu pia wasikose ajira
No comments:
Post a Comment