
Bei ya korosho msimu wa
2017 imeendelea kupanda mkoani Mtwara huku ikivunja rekodi ya tangu zao hili
kuwepo hapa Mkoani. Katika minada iliyofanyika leo mkoani hapa bei ya juu ya korosho
imeuzwa shilingi 4,007 kwa kilo wakati bei ya chini ikiwa shilingi 3880.
Bei ya juu ya korosho
iliyowahi kufikiwa mkoani hapa ni ilitokea msimu wa 2016/2017 ambapo bei ya juu
ya korosho ilifikia shilingi 4000 wakati uzalishaji ukiwa umepanda hadi kufikia
tani 172,771.109
tofauti na tani 106,940.222 zilizokuwa
zimezalishwa msimu wa 2015/2016.
Akizungumza na mwandishi
wetu Kaimu Katibu Tawala Msaidizi Mkoa wa Mtwara anaeshughulikia uchumi na
uzalishaji, Amani Lusake amesema katika mnada uliofanyika katika kijiji cha Mihambwe
leo Chama cha Ushirika cha Tandahimba na Newala (TANECU) kimeuza tani 10,000 ambapo
bei ya juu ya korosho imeuzwa kwa shilingi 4,007 wakati bei ya chini ni
shilingi 3970.
Kwa upande wa Chama cha
Ushirika cha Masasi na Mtwara (MAMCU) zimeuzwa tani 16,831.7 ambapo bei ya juu
imefikia shilingi 3985 wakati bei ya chini ikiwa ni shilingi 3880.
Bei hii ya korosho ni alama
na hatua muhimu ya mafanikio katika kilimo cha Korosho ambacho ni muhimu kwa
maendeleo ya Mkoa wa Mtwara.
No comments:
Post a Comment