Mfumo
wa Uhasibu na utoaji wa taarifa za fedha ngazi ya kituo cha kutolea huduma
(FFARS) umetajwa kuwa muarobaini wa matatizo mengi ya taarifa za matumizi ya
fedha zikiwemo za Elimu bure. Kupitia mfumo huu fedha zote zinazotumwa ngazi ya
vituo vya kutolea huduma kutoka serikalini zitakuwa zikionyeshwa katika mfumo
mmoja ambao utamuwezesha mfuatiliaji kutambua kasoro kwa urahisi.
Mafunzo
ya mfumo huu ambayo yanatolewa kwa udhamini wa watu wa Marekani kupitia mradi
wake wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) kwa watendaji ngazi ya
halmashauri hapa nchini unalenga kuondoa changamoto ya utoaji wa taarifa na
utambuzi wa matumizi ya fedha ambazo zimekuwa zikitolewa na serikali kwa watoa
huduma kama vile shule, hospitali na zahanati hapa nchini.
Akizungumza
na mwandishi wetu Wakati wa mafunzo haya yanayoendelea katika ukumbi wa Tiffany
Diamond Hotel mjini Mtwara leo, mmoja wa wanasemina Sarah Machumu ambaye pia ni
Afisa usimamizi wa fedha Ofisi ya Mkuu wa mkoa Dar es Salaam anasema mfumo wa
zamani unaotumika hadi sasa unachangamoto nyingi ikiwemo kutofanana kwa mfumo kati
ya halmashauri moja na nyingine hali ambayo inaleta shida katika ufuatiliaji na
utoaji wa taarifa za pamoja.
Anasema
awamu ya tano ya uongozi wa serikali imekuja na utaratibu mpya wa Elimu bila
malipo ambapo fedha zinatumwa moja kwa moja kwa watoa huduma hali ambayo
inaibua changamoto ya usimamizi na utoaji wa taarifa ya hizo fedha.

Kwa
upande wake Mhasibu wa Hospitali ya wilaya ya Rushoto Mwantumu Mbarouk anasema
kupitia mfumo unaotumika sasa kumebainika kuwepo na changamoto nyingi hasa kwa
watoa huduma. Sababu kubwa ya changamoto hizo ni pamoja na ufahamu mdogo wa
masuala ya fedha hali ambayo imekuwa ikisababisha makosa mbalimbali katika
utoaji wa taarifa.
Mwantumu
anasema mafunzo haya yamekuja kwa Wakati muafaka hasa katika kipindi hiki
ambacho serikali ya awamu ya tano imekuja na utaratibu wa kutuma fedha moja kwa
moja kwa vituo vya utoaji wa huduma zikiwemo shule za msingi na sekondari. Kupitia
mafunzo ya mfumo huu mpya itasaidia kupata njia muafaka ya kusimamia na kuandaa
bajeti ya mapato na matumizi ya fedha hizo na hata kuyatolea taarifa.
Awali
akifungua mafunzo haya yanayofanyika katika ukumbi wa Tiffany Diamond Hotel mjini
Mtwara leo, Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara, Elias Nyabusani anasema mafunzo
haya yatasaidia kuondoa kasoro nyingi zikiwemo zile za ukaguzi. Anasema baadhi
ya kasoro za ukaguzi wa fedha zilikuwa zikitokana na mapungufu ya kimfumo hasa
katika suala la kurekodi na kutoa taarifa za mapato na matumizi ya fedha. Anasema
katika kipindi hiki ambacho maendeleo ya kiteknolojia yamekuwa hasa katika
matumizi ya simu mafunzo haya yatasaidia kuzisogeza taarifa za kiganjani. Amesisitiza
watendaji kuwa makini katika kuhakikisha wanayatumia mafunzo haya kutatua
changamoto zinazowakabili.
Desideri Joseph Wengaa mtaalamu wa
mifumo ya TEHAMA na Mawasiliano kutoka mradi wa PS3
Akielezea
malengo ya mafunzo haya mtaalamu wa mifumo ya TEHAMA na Mawasiliano kutoka
mradi wa PS3 Desideri Joseph Wengaa anasema mafunzo haya ambayo yanatambulika kwa
lugha ya kiingereza kama ‘Fasility Financial Account and Reporting System’
(FFARS) yanalenga kuisaidia serikali kuisimamia masuala ya kifedha kwa vituo vya
kutolea huduma, Kama vile zahanati, shule na hospitali kwa lengo la kuhakikisha
fedha zinazotolewa zinafanya kazi katika malengo yaliyokusudiwa na kuweka uwazi
na uwajibikaji.
Anasema
mafunzo haya yanaendeshwa nchi nzima huku kanda ya Mtwara ikiwakutanisha mikoa
ya Mtwara, Lindi, Ruvuma, Pwani, Dar es Slaam na Tanga. Amefafanua kuwa mafunzo
haya yanatolewa kwa Wahasibu na wasimamizi wa fedha ngazi ya halmashauri na mikoa
kwa lengo la kuwawezesha kwenda kuwafundisha watoa huduma ambao wako katika
shule, hospitali na zahanati.
Video ya Tukio zima Bonyeza HAPA
Video ya Tukio zima Bonyeza HAPA
No comments:
Post a Comment