Kampeni kubwa iliyoanzishwa na uongozi wa mkoa wa Mtwara ya kuvutia wawekezaji inaendelea kuonesha nyota njema. Kiwanda cha kisasa cha kuchakata taka za aina zote zinazozalishwa hapa mkoani kujengwa katika Manispaa ya Mtwara Mikindani. Teknolojia ya kiwanda hiki itakuwa ya
kwanza hapa nchini.
Utambulisho wa wa teknolojia ya kiwanda hiki umefanyika leo katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara kupitia kampuni ya SBS ambayo imekuwa ikifanya kazi zake hapa nchini.
Viongozi wa mkoa na Manispaa wamenena na kuonesha ushirikiano mkubwa kwa wawekezaji hawa. Licha ya kwamba wawekezaji hawa watasaidia kusafisha mji, pia wataongeza ajira na bidhaa mbalimbali ikiwemo mkaa, mafuta yanayoweza kufanya kazi kama Dizeli, mbolea na takataka zingine.
Isikilize video hii ili upate kila kitu
No comments:
Post a Comment