MTWARA RS

FUATILIA TAARIFA MBALIMBALI ZINAZOHUSU MKOA WA MTWARA NA SEHEMU NYINGINE NDANI NA NJE YA TANZANIA, KWA MAWASILIANO E-mail: yustace.evaristy@mtwara.go.tz SIMU: +255 717 697 205

Wednesday, 9 November 2016



RC afuatilia changamoto za korosho Mtwara
Hii ni ishara njema ya mwaka wa kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa John Pombe Magufuli. Mara alipopanga safu yake ya uongozi hakufanya mabadiliko katika nafasi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mheshimiwa Halima Dendego pamoja na Katibu Tawala wa Mkoa Alfred Luanda.

Tafsiri ya hili ni kwamba bado alikuwa na imani kubwa kwa wawili hawa katika kuleta mabadiliko makubwa Mkoani Mtwara. Moja ya ahadi kubwa waliyoitoa kwa wanaMtwara ni kuleta mabadiliko chanya kwa kilimo cha Korosho ambacho ndicho muhimili wa uchumi wa Mtwara. 

Tangu kilimo cha korosho kifanyike mkoani Mtwara korosho ilikuwa haijawahi kufika shilingi 3000. Kwa mara ya kwanza katika historia ya kilimo cha korosho imepanda hadi 3830.

Pamoja na mazuri hayo bado kumeibuka changamoto ya ucheleweshaji wa malipo ya fedha kwa wakulima jambo ambalo leo limewaamusha wawili hawa wakiambatana na baadhi ya viongozi wa sekretarieti ya Mkoa, kamanda wa Polisi Mkoa, Mameneja wa Benki za CRDB na NMB ambako ndiko ziliko akaunti za wakulima wa Korosho mkoani Mtwara, Meneja wa Chama Kikuu cha Ushirika cha Masasi na Mtwara (MAMCU) kutembelea maghala, vyama vya Msingi na kuongea na wananchi.  

Msafara huu uliungana na uongozi wa Wilaya ya Masasi kwa Upande wa masasi na uongozi wa nanyumbu kwa Upande wa Nanyumbu.



Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mheshimiwa Halima Dendego akizungumza na viongozi wa Mkoa na Wilaya ya Masasi mara baada ya kupokea taarifa.









moja ya changamoto iliyotajwa na viongozi wa MAMCU ni suala ya unyaufu ambapo korosho imekuwa ikiongezeka uzito ama kupungua inaposafirishwa kutoka ghala la Chama cha Msingi kwenda Ghala Kuu. wajumbe walichangia kuwa ubora wa mizani pia unaweza kuwa unachangia kutokea kwa changamoto hizo hasa ikizingatiwa kuwa mizani inayotumika kwenye Vyama vya Msingi ni mizani ya mawe wakati Kwenye Ghala Kuu hutumia mizani ya digitali

Mheshimiwa Dendego (mwenye kitambaa kichwani) akikagua ghala kuu la BUCO Masasi. Moja ya changamoto iliyoripotiwa ni kuchelewa kusafirisha korosho iliyonunuliwa kutoka Ghalani. pamoja na uwepo na nafasi ya kutosha kuendelea kupokea korosho hapo gharani, Mheshimiwa ameagiza ndani ya wiki moja korosho zote ziwe zimesafirishwa kutoka maghalani. aidha kabla ya mnada ujao kusiwepo na korosho yoyote maghalani.

Wananchi wa kijiji cha Namagulumvi wakimsikiliza Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara. Wananchi wameonesha imani kubwa kwa Mheshimiwa. wameeleza kuwa mapambano aliyoyaanzisha kupambana na ununuzi na uuzaji haramu yamesaidia kwani hivi sasa wezi hawapo.

No comments:

Post a Comment