Pamoja sifa nyingi anazozipokea Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Halima Dendego Mkoani hapa ya Kuvunja rekodi ya bei ya korosho ambapo imepanda hadi shilingi 3837 kwa kilo, ziara yake imeendelea ambapo ametembelea maeneo mbalimbali Wilayani Newala, Tandahimba na Mtwara kwa lengo na kutatua changamoto wanazokutana nazo wakulima katika kipindi hiki cha kuelekea mwisho wa mauzo ya korosho.
Mkuu wa Mkoa Mtwara akipokea taarifa toka kwa Katibu wa Chama cha Msingi Naliendele kilichoko Wilayani Mtwara. Kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mheshimiwa Khatibu Malimi Kazungu
Mkuu wa Mkoa Mtwara akipokea taarifa toka kwa Katibu wa Chama cha Msingi Naliendele kilichoko Wilayani Mtwara. Kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mheshimiwa Khatibu Malimi Kazungu
Mkuu wa Wilaya ya Newala Mhe. Aziza Mangosongo akiwasilisha taarifa ya mwenendo wa Msimu wa Korosho 2016/2016 zoezi lililofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Newala.
Pamoja na mambo mengine alibaisha changamoto ya ucheleweshaji wa malipo ya fedha kwa wakulima kutokana na wakulima wengi kutokuwa na akaunti benki.
Mhe. Mkuu wa Mkoa ameagiza Mameneja wa Benki kuambatana na vikosi vya Maafisa wa serikali na vyama vya Msingi wakati wa ugawaji wa fedha vijijini ili akaunti zifunguliwe hukohuko. Aidha ameagiza zoezi la ugawaji lifanyike kama oparasheni maalumu ili kuhakikisha mkulima anapata fedha yake kwa haraka.
Baadhi ya magari yakisubiri kushusha na kuchukua korosho kutoka ghala la Agro-Focus Wilayani Newala.
Kufuatia hali hiyo Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa ameagiza ndani ya saa 48 wanunuzi wote ambao korosho yao iko ndani ya maghala makuu wawe wameiondoa ili kuruhusu korosho kutoka maghala ya vyama vya msingi kuingia.
Aidha, ndani ya wiki mbili wakulima wote wawe wameshafikisha korosho yao ndani ya Maghala Makuu. Hii itasaidia kuwahi bei sokoni.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Halima Dendego akizungumza na viongozi wa kiwanda cha kubangua korosho cha Micronix Wilayani Newala mara alipotembelea kiwandani hapo.
Kiwanda hiki kilibinafsishwa na Serikali kikiwa na uwezo wa kubangua tani 10000 kwa mwaka. kwa sasa hakifiki hata nusu ya uwezo.
Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa ameahidi kutuma wataalamu kuchunguza sababu walizozitoa kuwa ni matatizo ya umeme wa uhakika, maji na ukosefu wa wafanyakazi. Aidha, ameahidi kuwa matatizo yote yanayohitaji jitihada za serikali yatashughulikiwa mara moja ili kuhakikisha kampeini ya mkoa ya kuhakikisha korosho yote inayozalishwa mkoani hapa, inabanguliwa hapahapa.
Kaimu Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji Amani Rusake akifafanua jambo. Kulia ni Afisa kilimo Mkoa, Geofrey Mwalembe.
Baadhi ya viongozi walioambatana na Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa na viongozi wa Wilaya ya Newala wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa
No comments:
Post a Comment