Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa
Mtwara, Renatus Mongogwela amewaongoza mamia ya wananchi wa Wilaya ya Nanyumbu
katika shughuli ya Usafi kimkoa uliofanyika katika Mji wa Mangaka wilayani
Nanyumbu. zoezi hili limefanyika ikiwa ni utekelezaji wa agizo la serikali la usafi kila jumamosi ya mwisho wa mwezi.
Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa Mtwara, Renatusi Mongogwela (wa
tatu kushoto, shati jeupe) akiwaongoza wananchi kuelekea uwanja wa CCM nanyumbu
ili kupata nasaha za mwisho baada ya zoezi la usafi.
katika zoezi hilo
lililohudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mbunge wa Jimbo la nanyumbu Dua
William Nkurua, Mongogwela amesisitiza zoezi la Usafi kuwa endelevu kwa ngazi zote.
Amesema haipendezi kusubiri viongozi kuwaamusha wanananyumbu kufanya usafi
Wakati wote wamesoma na wanatambua kuwa usafi ni afya.
Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa
wa Mtwara, Renatus Mongogwela akihutubia wananchi mara baada ya usafi.
Sambaba na usafi huo
Mongogwela amewaongoza wana Nanyumbu
kupanda miti katika chanzo cha maji yanayohudumia vijiji vya Mara,
Sengenya na Ngalinje.
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara Renatus Mongogwela akipanda Mti katika chanzo cha maji cha Mara, Sengenya na Ngalinje.
Mbunge wa jimbo la Nanyumbu Dua
William Nkurua akipanda Mti.
Mhandisi wa mazingira mkoa,
Falaura Kikusa akipanda Mti.
Mbunge wa jimbo la Nanyumbu Dua
William Nkurua (wa kwanza kushoto)akiwasalimia wananchi mara abaada ya
zoezi la usafi.
Diwani wa kata ya Sengenya (mwenye
gauni jekundu) akiwasalimia wananchi mara baada ya usafi wa mazingira.
inawezekana pakafugwa samaki katika hilo bwawa na kupunguza uwezekano wa kukumbwa na balaa la ukosefu wa chakula ?
ReplyDeleteWataalamu wa Uvuvi wanaweza kuangalia japo lengo lake halikuwa kwa ajili ya samani bali huduma ya maji kwa wakazi
ReplyDelete