Mtwara ni jina la mji na mkoa wa Tanzania.
Mkoa wa Mtwara ni kati ya mikoa 26 ya Tanzania. Uko katika
pembe ya kusini-mashariki kabisa ya nchi. Umepakana na Mkoa wa Lindi upande wa
kaskazini, Bahari Hindi kwa mashariki, Msumbiji katika kusini na Mkoa wa Ruvuma
upande wa Magharibi. Mpaka wa kusini ni Mto Ruvuma.
Ukiwa na 16,720 km² Mtwara ni mkoa mdogo katika Tanzania
pamoja na Kilimanjaro.
Wakazi
Jumla kuna wakazi 1,128,523 (sensa 2002). Wanawake wanazidi
wakiwa 53 ya wakazi wote kwa sababu wanaume wengi hutoka nje kutafuta kazi.
Kati ya makabila ya Mtwara, Wamakonde wanajulikana zaidi
kutokana na sanaa yao ya uchongaji wa ubao hasa mpingo.
Utawala
Kuna wilaya 5: Mtwara Mjini (pia huitwa
"Mikindani"), Mtwara Vijijini, Masasi, Nanyumbu, Newala na
Tandahimba. Ndani yake kuna tarafa 21, kata 98 na vijiji 554.
Uchumi
Mtwara iko kati ya mikoa iliyobaki nyuma miaka mingi
kutokana na ugumu wa mawasiliano na barabara isiyopitika kwa sehemu kubwa .
Historia ya Mtwara inakuja sambamba na kumbukumbu ya jaribio
la Waingereza la kuanzisha mradi mkubwa wa maendeleo katika eneo hili
ulioshindikana kabisa.
Kuanzia 1947 serikali ya kikoloni ilijenga bandari ya Mtwara
pamoja na reli. Vilevile Mji wa Mtwara ulipangwa vizuri kwa ukubwa. Sababu yake
ilikuwa mpango wa kuanzisha kilimo cha mashamba makubwa kwa ajili ya karanga
hasa zilizohitajika kwa ajili ya mahitaji ya Waingereza ya mafuta ya kupikia.
Mradi huu ulishindikana kabisa, pesa nyingi ilipotea hadi
mradi ulifutwa kabla ya Tanzania kupata uhuru. Reli imeondolewa tena 1963.
Bandari imebaki ambayo haijaona kazi nyingi lakini bado ina
faida ya kuwa na nafasi nzuri sana ya kupokea meli kubwa. Wakati wa mapambano
dhidi ya serikali ya ubaguzi wa rangi Afrika Kusini, mipango mbalimbali ilitungwa
kutengeneza njia ya kupeleka bishaa kutoka bandari ya Mtwara kwenda Songea na
kutoka huko hadi Malawi kwa kuvuka Ziwa Nyasa.
Baada ya kujengwa kwa daraja la mto Rufiji mwaka 2002 kuna
matumaini mapya ya kuwa na barabara inayotumika kati ya Mtwara na Dar es Salaam.
Eneo la Mnazi Bay lina gesi inayoweza kutumika kwa mahitaji
ya nishati ya eneo lote. Tegemeo kubwa la uchumi kwa mkoa wa mtwara ni kilimo
hasa ikitegemea zao la korosho kwa wakulima wa wilaya zote za mkoa wa mtwara, kwa
miaka ya karibuni wilaya ya TANDAHIMBA na masasi ndio wamekuwa wazalishaji wa
kiwango cha juu wa korosho.
Pia mfumo wa stakabadhi ghalani umesaidia kwa kiasi fulani
kwa miaka ya awali ya uanzishwaji mfumo huo(msimu wa 2008/2009)kwa miaka
iliyofuata vyama vya msingi vimeonekana kuelemewa na mfumo huo na kusabaisha
sintofahamu inayoweza kurekebishwa kwa kuwahusisha wadau wote wa zao la
korosho.
No comments:
Post a Comment