MTWARA RS

FUATILIA TAARIFA MBALIMBALI ZINAZOHUSU MKOA WA MTWARA NA SEHEMU NYINGINE NDANI NA NJE YA TANZANIA, KWA MAWASILIANO E-mail: yustace.evaristy@mtwara.go.tz SIMU: +255 717 697 205

Thursday 29 August 2019

DC Walyuba awataka wananchi kujiandaa na uchaguzi Mkuu.


 Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe. Sebastian Waryuba amewataka wananchi wa Wilaya ya Tandahimba kujiandaa na uchaguzi wa serikali za Mitaa. wito huo ameutoa wiki hii katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Mchichira kata ya Mchichira Tarafa ya Mchichira wilayani hapo.
Amesema uchaguzi wa serikali za Mitaa unatarajiwa kufanyika Novemba 24, 2019 hivyo wananchi wanapaswa kujiandaa kuhakikisha wanashiriki kikamilifu ili kuwapata viongozi bora.

“Wananchi hakikisheni mnatumia haki yenu kuchangua viongozi bora. Hawa ndio mtawapa mamlaka ya kuwaongoza katika kujiletea maendeleo” amesema Walyuba

 Aidha, Mhe. Waryuba amewaambia wakulima wa korosho ambao bado hawajapata pesa zao kuwa watapatiwa pembejeo kwa asilimia mia moja bila kutoa malipo yoyote na kwamba wakishapatiwa pesa zao ndipo watakapolipa madeni hayo.

Katika mkutano huo uliohudhuriwa na umati mkubwa wa watu Mheshimiwa Waryuba ameuvunja uongozi wa kikundi Cha wakulima cha Mpunga maji ambacho kimeshindwa kuuendesha mradi wa mashine ya kukoboa mpunga ulioanzishwa na serikali kwa lengo la kuongeza thamani ya zao la mpunga na kuinua kipato cha wakulima.

Amesema viongozi hao wameshindwa kuendana na kasi ya serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe. Dkt John Pombe Magufuli kwani wamekuwa wakisababisha  migogoro isiyokwisha.

No comments:

Post a Comment