MTWARA RS

FUATILIA TAARIFA MBALIMBALI ZINAZOHUSU MKOA WA MTWARA NA SEHEMU NYINGINE NDANI NA NJE YA TANZANIA, KWA MAWASILIANO E-mail: yustace.evaristy@mtwara.go.tz SIMU: +255 717 697 205

Saturday 14 July 2018

Maadhimisho ya Wiki ya Elimu Mkoa wa Mtwara



Jana Juni 14, 2018 Mkoa wa Mtwara umeadhimisha Wiki ya Elimu kimkoa Mjini Tandahimba. Katika maadhimisho hayo Mgeni Rasmi Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa amewataka Wakurugenzi na Wakuu wa Wilaya kuhakikisha katika mipango yao ya ujenzi wa shule za kidato cha sita walenge kujenga shule za Mchepuo wa sayansi. Amesema kwa kuanzisha shule za mchepuo huo kutawavutia wanafunzi wengine kusoma masomo hayo kutokana na hamasa ya wenzao. Pia itasaidia kuondoa tatizo la walimu wa masomo hayo. kinachotakiwa ni viongozi kudhamiria na kuhakikisha mahitaji yote ya ujenzi wa shule zenye sifa hizo wanayatekeleza.

Kwa upande wa vyumba vya madarasa, amesema wameanza na utatuzi wa tatizo hilo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara ambapo shule 10 ambazo wanafunzi wake walikuwa wanasomea chini ya miti zimejengewa vyumba vya madarasa, Ameagiza kila Mkurugenzi ahakikishe anaondoa changamoto hiyo katika eneo lake.

Vilevile amepiga marufuku kusajili shule ambazo hazina vigezo. Ameeleza kuwa mapungufu mengi ya vyumba vya madarasa na ofisi za walimu yametokana na wenye jukumu la usajili wa shule hizo kutofuata vigezo. Amewataka wasikubali kushinikizwa na wanasiasa kwa matamanio yao ya kisiasa.


Vijana wa chipukizi wakipita kwa heshima mbele ya Mgeni Rasmi.


Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara Alfred Luanda akimkabidhi zawadi ya kikombe maalumu Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Byakanwa ikiwa ni ishara ya kutambua mchango wake mkubwa katika kuleta mabadiliko chanya kwenye sekta ya elimu Mkoani Mtwara


Afisa Elimu Mkoa, Germana Mung'aho akimuonesha Mkuu wa Mkoa Baadhi ya Vikombe vya mashindano ya UMISETA na UMITAMSHUMTA vilivyoletwa na wanafunzi wa Mkoa wa Mtwara katika mashindano yaliyofanyika kitaifa 2018 mjini Mwanza.

 
Mgeni Rasmi akikagua banda la mradi wa Tusome Pamoja. Mradi huu umesaidia kwa kiasi kikubwa kuleta mageuzi ya elimu mkoani Mtwara kwa kuweka misingi madhubuti ambayo imewezesha watoto kujua Kuandika, Kusoma na Kuhesabu katika hatua za awali.


 
Mtoto mwenye ulemavu wa akili akionesha maarifa katika kupangilia herufi na namba kupitia muongozo wa kujifunzia.


 Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara Mhe. Ahmad Said Chingoda akipokea zawadi ya Halmashauri bora kwa Mkoa wa Mtwara. Halmashauri hiyo ilikuwa ya kwanza kimkoa katika mtihani ya darasa la saba 2017 huku ikishika nafasi ya 64 kati ya Halmashauri 195 Tanzania.

 
Timu ya Mpira wa wavu (Volleyball) ambayo imeshika nafasi ya pili kitaifa UMISETA 2018 ikiwa katika picha pamoja na uongozi wa Mkoa (nyuma)

 
Bingwa wa kucheza bao mashindano ya UMISETA kitaifa 2018 Said Bakari (katikati). Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mheshimiwa Gelasius Byakanwa pamoja na Mwenyekiti CCM Mkoa wa Mtwara, Yusuph Said Nannila

 
Elimu ya Ujasiliamali na kilimo bora

 
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelaius Byakanwa akivaa kofia ngumu tayari kukabidhi Pikipiki zilizotolewa na Serikali kwa ajili ya waratibu Elimu Kata. Zoezi hili lilifanyika Julai 14, 2018 wakati wa kilele cha maadhimisho ya wiki ya Elimu iliyofanyika kimkoa wilayani Tandahimba

No comments:

Post a Comment