MTWARA RS

FUATILIA TAARIFA MBALIMBALI ZINAZOHUSU MKOA WA MTWARA NA SEHEMU NYINGINE NDANI NA NJE YA TANZANIA, KWA MAWASILIANO E-mail: yustace.evaristy@mtwara.go.tz SIMU: +255 717 697 205

Friday, 29 June 2018

Mgogoro wa Mpaka uwanja wa Ndege Mtwara waundiwa Tume

Wiki hii Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mheshimiwa Gelasius Byakanwa amefanya ziara katika Halmahauri ya Manispaa ya Mtwara Mikindani kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na kusikiliza kero zinazohusiana na masuala ya ardhi. Ziara hiyo ya siku mbili ilianza tarehe 27 na kukamilika tarehe 28.


Moja ya mgogoro aliousikiliza ni kuhusu mpaka kati ya makazi ya wananchi na eneo la uwanja wa ndege.

Baada ya kusikiliza pande zote Mheshimiwa Byakanwa ameunda Kamati Maalumu ambayo ameiagiza kupitia nyaraka zote za migogoro hiyo na kumshauri nini kifanyike.

Hapa ni baadhi ya matukio yaliyojitokeza katika ziara hiyo;
   Mheshimiwa Byakanwa akipokea nyaraka za utetezi toka kwa Meneja wa Uwanja wa Ndege Emily Simbachawene


2. Mheshimiwa Byakanwa akikagua ujenzi wa ofisi ya Mtendaji wa Kata Jangwani. Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara mikindani imeweza kujenga ofisi za watendaji kwa kata zote 18 zinazounda Halmashauri hiyo.
Mheshimiwa Byakanwa akimzawadia fedha taslimu mwalimu Issa Dengi wa shule ya msingi Singino ambaye somo lake la Kiswahili liliongoza kiwilaya katika mtihani wa Taifa wa Kiswahili darasa la saba 2017.
Ujenzi wa kituo cha mabasi Mkanaledi. 
Ujenzi huu unakusudia kuondoa changamoto ya mlundikanao wa magari katika kituo cha sasa kilichoko Mtwara mjini ambacho kinapokea magari yanayoenda mikoani/Wialayani na daladala.
 
Mheshimiwa Byakanwa akipokea maelezo ya ujenzi wa ukuta wa ofisi Mkurugenzi wa Manispaa. 

Ujenzi huu unakusudia kuimarisha usalama wa ofisi na kupunguza muingiliano wa watumishi na watu wa nje.


     Ujenzi wa zahanati Mbawala chini.  
  Wananchi wametoa ardhi ekali 5, kusaidia nguvu kazi kwa ajili ya ujenzi wa zahanati hiyo. 
 Mheshimiwa Byakanwa akiwazawadia fedha taslimu wanafunzi wa shule ya Msingi Singino waliojibu kwa ufasaha maswali ya chemsha bongo aliyowauliza wakati wa ziara hiyo

  Mwenyekiti wa Mtaa wa Mbawala Chini (katikati) pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mheshimiwa Gelasius Byakanwa (Kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhehimiwa Evod Mmanda mara baada ya ukaguzi wa ujenzi wa Zahanati.

No comments:

Post a Comment