Amesema lengo la kuanzishwa kwa majeshi yote ni kutoa huduma kwa
wananchi wa Tanzania hivyo mshikamano ni jambo la muhimu.
Akizungumzia Jeshi la Wananchi wa Tanzania amesema Jeshi hilo
kama linavyojulikana ni jeshi ambalo limetokana na watanzania wenyewe hivyo
linapaswa kuenzi malengo ya waasisi ambayo ni pamoja na uzalendo.
Katika maazimisho hayo yaliyojumuisha majeshi mbalimbali ya
hapa nchini Msongole amesema historia ya jeshi la Wananchi wa Tanzania ilianzia
tangu likiitwa King African Rifle ambalo lilianzishwa na Mkoloni kwa lengo la
kulinda maslahi ya mkoloni kisha kubadilishwa kuwa Tanganyika Rifle na hatimaye
Jeshi la Wananchi wa Tanzania lililoanzishwa Septemba 1, 1964.
Msongole amesema
majeshi yote yanapaswa kutambua kuwa malengo yao ni ustawi wa taifa na hivyo
kuacha tofauti zao na kuwa kitu kimoja.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mheshimiwa Halima
Dendego amelishukuru Jenshi la Wananchi wa Tanzania na majeshi yote kwa
ushirikiano wao katika kufanikisha shughuli hiyo. Amesema yako mengi
yaliyofanywa na Majeshi hapa Mtwara ambayo yanabaki kama kumbukumbu kwa taifa. Ametaja
baadhi ya mambo hayo kuwa ni pamoja na ujenzi wa miundombinu ya usalama wa
kituo cha kuzalisha Umeme eneo la Pwani ya Mnazi mara baada ya mafuliko ya
bahari yaliyotishia usalma wake mwanzoni mwa mwaka 2015.
Sherehe hizi zilitanguliwa na maandamano ya kilometa 10
ambapo raia waliungana na wanajeshi katika matembezi hayo kisha kuendesha zoezi
la Upimaji wa Virusi vya Ukimwi na uchangiaji damu kwa hiari.
Video ya Tukio zima Hii Hapa.
No comments:
Post a Comment