MTWARA RS

FUATILIA TAARIFA MBALIMBALI ZINAZOHUSU MKOA WA MTWARA NA SEHEMU NYINGINE NDANI NA NJE YA TANZANIA, KWA MAWASILIANO E-mail: yustace.evaristy@mtwara.go.tz SIMU: +255 717 697 205

Friday, 2 June 2017

Nanenane kitaifa Ngongo, maandalizi motomoto

Mikoa ya Mtwara na Lindi imeendelea na maandalizi ya maonesho ya wakulima maarufu kama Nanenane yanayotarajiwa kufanyika Kitaifa katika viwanja vya Ngongo vilivyoko Lindi Agost 2017. 

 Wajumbe wakifuatilia mijadala wakati wa kikao cha maandalizi. Mwenye Kitambaa Kichwani ni Mkuu wa Wilaya ya Newala Mhe. Aziza Mangosongo

Akizungumza baada ya kikao cha maandalizi kilichofanyika jana katika ukumbi wa Naliendele ulioko uwanjani hapo, Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mheshimiwa Godfrey Zambi amesema taratibu zote za maandalizi zinaenda vizuri. 


Wajumbe kutoka mikoa yote miwili wanaonesha moyo  hali ambayo inaashiria uwezekano wa maonesho ya mwaka huu kuwa mazuri kuliko yote yaliyowahi kufanyika.
  
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mheshimiwa Godfrey Zambi akizungumzia maandalizi ya Maonesho hayo

Mheshimiwa Zambi amesema miezi kadhaa nyuma eneo la viwanja hivyo lilikuwa katika hali isiyoridhisha lakini sasa hali ni nzuri na kila kukicha mabadiliko zaidi yanaendelea kuonekana.

Mwandishi wetu ameshuhudua Wakuu wa Wilaya na Wakutrugenzi wa halmashauri za wilaya mbalimbali katika mikoa hii miwili wakikagua maeneo ya halmashauri zao hali ambayo inaashiria uwezekano wa mambo kuwa mazuri zaidi kwa wakati.

Mikoa ya Mtwara na Lindi itakuwa ikiandaa kwa mara ya nne mfululizo maonesho haya katika ngazi ya kitaifa. Aidha katika maonesho ya mwaka jana Mgeni rasmi katika ufungaji wa maoenesho hayo alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suruhu Hassan.

No comments:

Post a Comment