Katika kuutafuta ukweli juu ya bandari ya Mtwara na hasa
katika kipindi hiki ambacho kelele nyingi zimesikika zikipinga kuwa bandari
hiyo ni ndogo kuweza kupokea na kusafirisha shehena ya korosho, Mwandishi wa
Mtwarars.blogspot.com leo ameamua kufanya ziara ya kushtukiza katika bandari
hiyo.
Moja ya jambo la kufurahisha na kushangazani pale meli mbili
kubwa zilivyokuwa zimepaki katika gati moja huku zote zikipakiwa na kushusha
makasha tayari kwa kusafirishwa nje ya nchi. Muonekano wa meli hizi katika gati
ya bandari hii zilipingana na simulizi nyingi za kupinga uwezo wa bandari hii.
Meli mbili kubwa zilizokuwa katika bandari ya Mtwara Wakati
mwandishi wetu alipotembelea eneo hilo. (Muonekano wote uko katika clip ya
video yenye mahojiano na viongozi wa bandari)
Akizungumzia uwezo wa bandari hiyo Kapteni Hussein Bakari Kasuguru
ambaye pia ni Baharia kiongozi wa bandari za mikoa ya kusini amesema bandari ya
Mtwara ina uwezo mkubwa kuhilimi mizigo yote inayosafirishwa kupitia bandari
hiyo.
Amesema meli yoyote yenye urefu wa mita kuanzia 180 ina uwezo
wa kutia nanga katika bandari ya Mtwara na kwamba bado eneo la ghati ya bandari
ni kubwa kuweza kuhimili meli mbili kwa Wakati mmoja. Aidha bandari hiyo ina
kina cha mita 9.5 ambayo pia ni sifa ya ziada ya kuifanya iwe moja ya bandari
bora duniani.
Kapteni
Kasuguru akizungumza na mwandishi wetu.
Kapteni Kasuguru ameeleza kuwa kutokana na sifa hiyo ndiyo
maana amethubutu kuweka meli mbili ambazo zikiunganishwa kwa pamoja zina urefu
wa futi 296.
‘Hiyo meli unayoiona ya Kota Nilam ina urefu wa futi 180
wakati meli hiyo ya Al Dhakhira ina
urefu wa mita 116. Ukijumlisha zote mbili unapata jumla ya mita 296. Kama
bandari isingekuwa na uwezo huo hivi sasa tungekuwa tunalaumiana mitaani kwamba
tumefanya lisilowezekana’. Amesisitiza kaptein Kasuguru.
Kapteni Kasuguru ambaye ana uzoefu wa miaka mingi katika kazi
hii amesisitiza kuwa siku zote duniani mataifa yanakuwa na utaratibu wake
katika kuendesha mambo.
‘Wakati wowote serikali ikiamua utaratibu lazima usingatiwe,
ndiyo maana sina wasiwasi na serikali ya Tanzania kuamua kutumia bandari ya
Mtwara ambayo mimi kama Kapteni mzoefu sikushangaa Wakati tamuko la kuitumia
bandari ya Mtwara kusafirisha korosho zote zinazotoka mikoa ya kusini’. Linatolewa.
Alisisitiza.
Afisa utekelezaji mwandamizi Bandari ya Mtwara Robert Soko.
Kwa upande wake Afisa utekelezaji mwandamizi Bandari ya
Mtwara, Robert Soko amesisitiza kuwa kasi ya usafirishaji wakorosho kwa musimu
wa 2016/2017 imeongezeaka.
Ameeleza kuwa mwezi Desemba, 23 mwaka 2015 walikuwa
wameshahudumia meli 10 wakati Desemba, 23 mwaka 2016 wameshahudumia meli 13.
Kwa upande wa shehena ya korosho, hadi Desemba, 23 mwaka 2015
walikuwa wameshasafirisha tani 67,000 wakati mwaka huu tayari wamefikia zaidi
ya tani 80,000. Aidha meli mbili zilizopo zinataraji kusafirisha jumla ya tani
20,000 na kufanya usafirishaji kufikia zaidi ya tani 100,000.
Soko anasisitiza kuwa kwa kawaida musimu wa usafirihaji wa
korosho kila mwaka huenda mpaka mwezi wa tatu lakini mwaka huu wamejipanga kuhakikisha
hadi katikati ya mwezi Januari wawe wamesafirisha zaidi ya tani 150,000. Kwa kiasi
hicho ni matarajio kuwa korosho yote inayotarajia kupitia bandari ya Mtwara
itakuwa imesafirishwa nje ya nchi.
Tazama video nzima hapa
Tazama video nzima hapa
No comments:
Post a Comment