Waziri wa Nishati Mheshimiwa Dkt. Medard Kalemani amewaka
watanzania kuchangumkia fursa
iliyotolewa na serikali ya kuuunganishiwa umeme kwa kutumia kifaa kinachojulikana
kama Umeme Tayari (UMETA). Amesema kifaa hicho kinamuepusha mtumiaji na gharama
za kufanya ‘wiring’ na hivyo kupunguza gharama za kuingiza umeme kwenye nyumba.
Waziri ameyasema hayo jana katika maeneo tofauti alipokuwa
katika ziara yake ya siku mbili mkoani Mtwara.
“Serikali imeamua kuwapungumzia
gharama wananchi kwani ukishaweka hicho chombo hulazimiki tena kufanya ‘wiring’
kwa nyumba za wastani, hasa nyumba zenye chumba kimoja hadi vinne. Kwa vile hicho kifaa kinafaa kwa matumizi
yote isipokuwa viwanda tunawashauri wnanchi wavitumie. Pia tunashauri vifaa
hivi vitumike kwenye taasisi za Umma kama ofisi za vijiji vituo vya afya, vituo
vya polisi, zahanati na maeneo mengine ambayo kimsingi si lazima sana ufanye
wiring.”
Amesisitiza kwamba serikali imewataka wakandarasi wahakikishe
wanavitoa kwa wateja wa kwanza mia moja hadi mia mbili hamsini. baada ya hapo
vinakuwa vinauzwa kwa bei ya serikali ambayo ni shilingi 36,000.
Kwa kuanzia amegawa vifaa hivyo katika majimbo yote
aliyotembelea ikiwemo Nanyamba, Newala na Lulindi.
Pamoja na punguza hilo amesema serikali bado inaendelea na
punguza la kuingiza umeme kupitia mradi wa REA ambapo gharama yake ni shilingi
elfu 27 tu kwa maeneo ya vijijini.
No comments:
Post a Comment