Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa Majaliwa
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassimu Majaliwa Majaliwa amewasimisha kazi Afisa Mipango wa Halmashauri ya Mji wa Masasi Teresia Msumba pamoja na Kaimu Mweka Hazina wa halmashauri hiyo Heri Hamadi kutokana na ubadhilifu wa zaidi ya shilingi bilioni 1.8 za ujenzi wa jengo la utawala la halmashauri hiyo ambalo halijaisha tangu mwaka 2014.
Aidha Mheshimiwa Majaliwa
ameagiza asakwe popote alipo aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo,
Fortunatus Kagoro ili wote kwa pamoja wahojiwe na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana
na rushwa TAKUKURU.
Mheshimiwa Mjaliwa
amechukua hatua hiyo wakati wa kikao na watumushi wa Halmashauri Wilayani Masasi
kilichofanyika katika viwanja vya Ikulu Ndogo Mjini Masasi.
Amesema fedha hizo
zilitolewa kwa nyakati tofauti na serikali Kuu kwa ajili ya ujenzi wa jengo la
utawala la halmashauri hiyo jambo ambalo halikutekelezwa kama ilivyoagizwa.
No comments:
Post a Comment