Chemba ya Wafanya biashara,
Wenye Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA) wamezindua Meli ya Biashara
itakayokuwa ikifanya safari zake kati ya Mji wa Mtwara, Tanzania hadi mjini Moroni
nchini Comoro. Zoezi hilo limefanyika jana katika eneo la bandari ndogo iliyoko
karibu na hotel ya Southern Cross zamani ikiitwa Msemo Hotel mjini Mtwara.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo ambao utaanza na meli ya VILLE DE
FOMBONI MOH 0022, Mwenyekiti wa TCCIA mkoa wa Mtwara Swallah Said Swallah
amesema kupatikana kwa usafiri huo ni suala ambalo wamelipigania kwa muda mrefu
ikiwani hatua muhimu ya kuunganisha wafanyabiashara wa mkoa wa Mtwara na wale
wa Comoro.
Amesema ziko sababu nyingi muhimu za kuruhusu biashara hiyo hasa
kutokana na jiografia ya maeneo haya mawili. Amesema umbali kutoka Mtwara hadi
Comoro ni kilomita 321 wakati nchi zingine ambazo zimekuwa zikifanya biashara
na Comoro ni kilomita zaidi ya 3000.
Amesema hadi mwaka 2016 Tanzania ambayo ndiyo kijiografia iko karibu zaidi
na Comoro ilikuwa ni ya 17 kati ya nchi ambazo zimekuwa zikifanya biashara na nchi
hiyo. Amezitaja nchi ambazo zimetawala soko hilo kuwa ni pamoja na Ufaransa,
Afrika Kusini, Nchi za Kiarabu, Madagasca na nchi zingine. Amewataka wananchi
wa Mkoa wa Mtwara kuchangamukia fursa hiyo ili kujiongezea kipato.
Kwa upande wake Mgeni Rasmi wa ufunguzi huo, Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe.
Evod Mmanda ambaye alikuwa akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mheshimiwa
Halima Dendego amesema kuna kila sababu ya Mkoa wa Mtwara kunufaika na biashara
hiyo kwani hakuna bidhaa ambazo zinahitajika Comoro ambazo hazipatikanani
Mtwara. Amesema mahitaji makubwa ya Comoro ni pamoja na mazao ya vyakaula kama
Nafaka, Magimbi, Viazi mbogamboga ambavyo vyote kwa pamoja vinapatikana Mtwara.
Mheshimiwa Mmanda amewataka wananchi wa Mtwara kuchangamukia fursa
badala ya kukaa wakaendelea kulalamika hatimaye soko hilo kutawaliwa na watu wa
nje ya mkoa.
Mwajuma. Mfanyabiashara
Kwa upande wao baadhi ya wananchi ambao wamekuwa wakifanya biashara na
nchi hiyo wamesema biashara ya bidhaa kutoka Tanzania kwenda Comoro inalipa.

Aidha mfanyabiashara aliyejulikana kwa jina moja la Mwajuma anasema amekuwa akipeleka korosho ambazo anazinunua
hapa mjini Mtwara kwa shilingi 20,000 kwa kilo lakini mjini Comoro bidhaa hiyo
huuzwa hadi shilingi elfu arobaini. Amewataka wananchi wa Mkoa wa Mtwara
kuchangamukia fursa ya biashara hiyo.
Video ya tukio hii hapa chini.
naomba namba ya dalali wa comoro kuhusu biashara ya mbogamboaga
ReplyDelete