MTWARA RS

FUATILIA TAARIFA MBALIMBALI ZINAZOHUSU MKOA WA MTWARA NA SEHEMU NYINGINE NDANI NA NJE YA TANZANIA, KWA MAWASILIANO E-mail: yustace.evaristy@mtwara.go.tz SIMU: +255 717 697 205

Monday 2 January 2017

Mamantilie Mtwara watamani musimu wa korosho uendelee miezi sita zaidi. Wadai faida wanayoipata ni kubwa.



Wakati musimu wa Korosho mkoani Mtwara ukielekea ukingoni akina mama wanaotoa huduma ya chakula kwa wabeba mizigo kwenye maghala ya kuhifadhia korosho wamepaaza sauti zao wakishukuru uwepo wa uchumi wa korosho.

Katika mahojiano maalumu na mtwarars.blogspot.com akina mama hao wametamani musimu wa korosho uwe unakuwepo kwa zaidi ya miezi sita. Aidha pato wanaloltapa limewasaidia kwa kiasi kikubwa kubadilisha maisha yao.


 Ingewezekana Musimu wa Korosho uwe unaendelea kwa kipindi cha zaidi ya miezi sita kwani manufaa yake ni makubwa kwetu. (Mwajuma Hassan)

Kwa siku napata faida hadi shilingi 20,000 lakini kama kungekuwa na makubaliano ya pamoja na wenzangu kwa siku ingekuwa zaidi. (Emmy Baraka)

Nikilinganisha Biashara ya maghalani na Mtaani. Maghalani napata faida kubwa hivyo tuwekewe miundombinu mizuri ya kutoa huduma (Halima Omari)

Ninachokipata si haba. kinanitosheleza. (Lukia Abdul)


pata Video yote hapa.

  



No comments:

Post a Comment