Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikiwa watu wenye Ulemavu, Mhe. Abdalla Possi akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Halima Dendego mara baada ya kuwasili Ofisini hapo.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia watu wenye ulemavu, Abdallah Possi ameitaka jamii kutoa elimu ili kuwasaidia wenye ulemavu kuishi kwa amani katika jamii. Amesema elimu hiyo inapaswa kutolewa katika vikao mbalimbali vya kijamii vikiwemo mikutano ya hadhara, semina na makongamano. Kufanya hivyo kutaondoa adha ya kulazimika kuwatenga wenye ulemavu kwenye mashule na huduma mbalimblai za kijamii kama inavyofanyika sasa.

Mheshimiwa Dakta Possi
ameyasema hayo jana katika ziara yake siku moja Wilayani Masasi Mkoani Mtwara.
Amesema zama hizi si kama
zama za zamani ambapo unyanyapaa ulikuwa wa hali ya juu hivyo jamii inapaswa
kuendeleza agenda ya haki na usawa kwa jamii.
Naibu Waziri, Mhe. Dakta Abdallah Possi akizungumza na walimu wa shule ya Msingi Masasi Maalumu hawapo pichani.

Akipokea taarifa ya shule ya
Msingi Lulindi maalumu iliyoko Wilayani Masasi amesema shule na vyuo vingi
vilivyoanzishwa miaka ya 70 Kwa sasa havina vifaa vya kuwezesha kufanya mafunzo
yaliyotarajiwa, hivyo serikali inapaswa kuangalia upya jinsi walemavu
wanavyoweza kupata mafunzo katika mifumo mingine iliyopo kuliko kung’angania
vyuo vilivyoandaliwa miaka hiyo wakati ni vichache, havina vifaa na havipo nchi
nzima.
Mkuu wa Wilaya ya Masasi Mhe. Seleman Mzee akimkaribisha Naibu Waziri katika shule ya Msingi Lulindi Maalum

Mheshimiwa Possi ambaye
kitaalumu ni Mwanasheria amesema viongozi wanapaswa kujiongeza kwa kuwa
wabunifu. Waache tabia ya kulalamika kuwa bajeti haitoshi.
‘Katika nchi inayoendelea
kama Tanzania kila mtu anategemea bajeti ya serikali. Kiongozi anapaswa kujiongeza
kwani wapo wadau walio tayari kusaidia. Wanachohitaji ni kushirikishwa kwa
kuwaandikia maandiko yenye kuanishwa mahitaji yaliyopo na umuhimu wake.
Waalimu wa Shule ya Msingi Lulindi Maalumu wakijitambulisha kwa Mheshimiwa Waziri
MHeshimiwa Abdallah Possi akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Mtwara. kutoka kulia ni Afisa Habari wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Evaristy Masuha. Mjumbe wa NEC wa chama cha mapinduzi wilaya ya Masai na Kaimu Muganga Mkuu wa Mkoa wa Mtwara,Telesia Ngonyani.

No comments:
Post a Comment