MTWARA RS

FUATILIA TAARIFA MBALIMBALI ZINAZOHUSU MKOA WA MTWARA NA SEHEMU NYINGINE NDANI NA NJE YA TANZANIA, KWA MAWASILIANO E-mail: yustace.evaristy@mtwara.go.tz SIMU: +255 717 697 205

Monday 6 April 2015

IJUE MTWARA

Mtwara ni jina la mji na mkoa wa Tanzania.

Mkoa wa Mtwara ni kati ya mikoa 26 ya Tanzania. Uko katika pembe ya kusini-mashariki kabisa ya nchi. Umepakana na Mkoa wa Lindi upande wa kaskazini, Bahari Hindi kwa mashariki, Msumbiji katika kusini na Mkoa wa Ruvuma upande wa Magharibi. Mpaka wa kusini ni Mto Ruvuma.

Ukiwa na 16,720 km² Mtwara ni mkoa mdogo katika Tanzania pamoja na Kilimanjaro.

Wakazi
Jumla kuna wakazi 1,128,523 (sensa 2002). Wanawake wanazidi wakiwa 53 ya wakazi wote kwa sababu wanaume wengi hutoka nje kutafuta kazi.

Kati ya makabila ya Mtwara, Wamakonde wanajulikana zaidi kutokana na sanaa yao ya uchongaji wa ubao hasa mpingo.

Utawala
Kuna wilaya 5: Mtwara Mjini (pia huitwa "Mikindani"), Mtwara Vijijini, Masasi, Nanyumbu, Newala na Tandahimba. Ndani yake kuna tarafa 21, kata 98 na vijiji 554.

Uchumi
Mtwara iko kati ya mikoa iliyobaki nyuma miaka mingi kutokana na ugumu wa mawasiliano na barabara isiyopitika kwa sehemu kubwa .

Historia ya Mtwara inakuja sambamba na kumbukumbu ya jaribio la Waingereza la kuanzisha mradi mkubwa wa maendeleo katika eneo hili ulioshindikana kabisa.

Kuanzia 1947 serikali ya kikoloni ilijenga bandari ya Mtwara pamoja na reli. Vilevile Mji wa Mtwara ulipangwa vizuri kwa ukubwa. Sababu yake ilikuwa mpango wa kuanzisha kilimo cha mashamba makubwa kwa ajili ya karanga hasa zilizohitajika kwa ajili ya mahitaji ya Waingereza ya mafuta ya kupikia.

Mradi huu ulishindikana kabisa, pesa nyingi ilipotea hadi mradi ulifutwa kabla ya Tanzania kupata uhuru. Reli imeondolewa tena 1963.

Bandari imebaki ambayo haijaona kazi nyingi lakini bado ina faida ya kuwa na nafasi nzuri sana ya kupokea meli kubwa. Wakati wa mapambano dhidi ya serikali ya ubaguzi wa rangi Afrika Kusini, mipango mbalimbali ilitungwa kutengeneza njia ya kupeleka bishaa kutoka bandari ya Mtwara kwenda Songea na kutoka huko hadi Malawi kwa kuvuka Ziwa Nyasa.

Baada ya kujengwa kwa daraja la mto Rufiji mwaka 2002 kuna matumaini mapya ya kuwa na barabara inayotumika kati ya Mtwara na Dar es Salaam.

Eneo la Mnazi Bay lina gesi inayoweza kutumika kwa mahitaji ya nishati ya eneo lote. Tegemeo kubwa la uchumi kwa mkoa wa mtwara ni kilimo hasa ikitegemea zao la korosho kwa wakulima wa wilaya zote za mkoa wa mtwara, kwa miaka ya karibuni wilaya ya TANDAHIMBA na masasi ndio wamekuwa wazalishaji wa kiwango cha juu wa korosho.


Pia mfumo wa stakabadhi ghalani umesaidia kwa kiasi fulani kwa miaka ya awali ya uanzishwaji mfumo huo(msimu wa 2008/2009)kwa miaka iliyofuata vyama vya msingi vimeonekana kuelemewa na mfumo huo na kusabaisha sintofahamu inayoweza kurekebishwa kwa kuwahusisha wadau wote wa zao la korosho.

No comments:

Post a Comment